MATUMIZI YA RANGI ZA MAPAA YA MAJENGO KATIKA KUBORESHA MUONEKANO WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA.
UTANGULIZI:
Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kuboresha mandhari ya mji ili kufikia malengo ya kuufanya mkoa wa Dodoma hasa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuwa mji wa kisasa unaoendana na miji ya kimataifa kuwa Makao makuu ya nchi.
Jiji likiwa ndio msimamizi mkuu wa Mipango miji na uboreshaji wake, linawajibika kuwafanya wananchi na taasisi zote kufuata mipango hiyo ili kukamilisha lengo la Dodoma kuwa mji wa kimataifa katika shughuli za kiserikali na kibiashara.
Mpango wa kupaka rangi mapaa ya majengo ni moja ya mikakati katika kuboresha muonekano wa jiji, itakayosaidia kupendezesha mji na kupata utofauti wa kipekee kwa maeneo husika.
MABORESHO YATAKAYOTUMIKA KATIKA RANGI YA KUPAUA AU KUPAKWA.
Mpango huu utahusisha kata zote 41 za Jiji la Dodoma ambapo matuminzi ya rangi zitakazotumika ni kama ifuatavyo;
• BLUU MPAUKO/BAHARI (LIGHT BLUE)
• KIJANI MPAUKO
• KIJANI ILIYOIVA (DEEP GREEN)
• KAHAWIA (BROWN/CHOCOLATE)
• NYEKUNDU MPAUKO (KAROTI)
Madhumuni ya mpango huu ni kuboresha muonekano na kuleta utambuzi wa kimaeneo na mvuto katika muonekano wa mitaa na kata zake zote.
Hivyo, matumizi haya ni kwa kata zote 41 kulingana na rangi husika ya kupaulia au kupakwa. Mpango huu utafanyika katika maeneo yote ambayo aidha vibali vya ujenzi vimeshatolewa au kwa maeneo ambayo hayana vibali vya ujenzi.
Kwa pamoja, mapaa ya majengo ya watu na taasisi zote ndani ya Jiji la Dodoma zitawajibika kuboresha muonekano huu. Serikali za kata na Mitaa husika kwa pamoja watashiriki katika mpango huu kwenye kubadilisha muonekano wa mapaa yao kama rangi ya kata husika ilivyopendekezwa.
Aidha katika kuboresha muonekano wa maeneo yote ambayo bado hayajatolewa vibali vya ujenzi, kutakuwepo na ongezeko la masharti ya ujenzi kwa waombaji juu ya aina ya rangi ya paa la jengo.
Bofya hapa kuona rangi kwa kila kata: RANGI ZA PAA KWA KILA KATA
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.