Na. Coletha Charles, DODOMA
Halmashauri ya Jiji la Dodoma imewatembeza Madiwani wa Halmashauri za Wilaya ya Igunga na Makete katika miradi ya maendeleo kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa Miradi, ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa taka ngumu na uwekezaji.
Akizungumza wakati wa kwenda kuzungukia Miradi hiyo, Afisa Mipango Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Rozalia Hhari, alitoa ufafanuzi wa Miradi iliyotekelezwa kwa fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mapato ya ndani ya Halmashauri, nguvu za wananchi na fedha za wahisani.
Alisema kuwa kunamiradi ambayo imekamilika na mingine bado inatekelezwa kama ujenzi wa Uwanja wa Ndege Masalato, Majengo ya Wizara, Treni ya Mwendo Kasi (SGR) na Barabara ya Mzunguko, ambapo kwa mwaka huu wanatengemea kukusanya mapato ya ndani shilingi Bilioni 62, lakini mwaka jana walikusanya Bilioni 58.
“Miradi tuliyokamilisha na inafanya kazi kwa sasa ni Kituo cha Mabasi kimegharimu thamani ya shilingi Bilioni 24.03, Soko la Wazi la Machinga shilingi Bilioni 9.5, Chinangali Park shilingi Bilioni 2.9, Nala roli park shilingi Bilioni 5.9, Shule ya English Medium Msangalale Milioni 750, Dodoma City Hotel Bilioni 11.9, Soko Kuu la Job Ndugai Shilingi Bilioni 14 na Mtumba Complex (ukumbi wa Mikutano) mradi ambao unatekelezwa kwa awamu tatu na gharama yake ni shilingi Bilioni 59, ila kwa awamu ya kwanza ishakamilikia ni Bilioni 18” alisema Hhari.
Naye, Diwani wa Kata ya nkinga Jimbo la Manonga Wilaya ya Igunga, Samwel Masanja, alisema kuwa wamejifunza mambo mengi katika Halmashuri ya Jiji la Dodoma na wataenda kuyafanyia kazi kwa uthubutu mkubwa katika wilaya yao waweze kukusanya mapato na kujenga miradi.
“Yale tuliyojifunza leo tumeona ni fursa katika kujifunza namna ya kukusanya mapato na kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Lakini tumeshea mambo mbalimbali na wenzetu wa Makete na wao wanakusanya vipi mapato na namna ya kuendesha Halmashauri ambapo tuki jumlisha yale tuliojifunza hapa yatakuwa na msaada” alisema Masanja.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.