• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

AfDB kulig'arisha jiji la Dodoma kwa barabara za kisasa; huduma za jamii

Imewekwa tarehe: August 20th, 2019

JIJI la Dodoma na vitongoji vyake, hivi karibuni litabadilika mwonekano wake na kuwa la viwango vya kimataifa baada ya Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB kuipatia Tanzania mikopo yenye masharti nafuu ya dola milioni 180 sawa na shilingi bilioni 414 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) kwa kiwango cha lami na uboreshaji wa miundombinu katika Jiji hilo.

Makubaliano ya mikopo hiyo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, kwa upande wa Serikali, na Meneja Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini, Bw. Alex Mubiru.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mikopo hiyo, Bw. Doto James, amefafanua kuwa mradi utahusisha Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa njia nne zenye urefu wa km 110.2 kwa kiwango cha lami kutoka Nala – Veyula – Ihumwa – Matumbulu.

Alisema mikopo hiyo pia inahusisha uboreshaji wa upatikanaji wa miundombinu ya huduma za kijamii ikiwemo huduma za maji na vituo vya afya; Ukarabati wa barabara za mchepuko; na Utekelezaji wa mikakati ya usalama wa barabarani katika mji wa Dodoma itakayotekelezwa katika kipindi cha miaka miwili” alifafanua Bw. James.

”Kupitia Mikataba hii, Benki ya Maendeleo ya Afrika itatoa kiasi cha dola za Marekani milioni 138 kupitia dirisha la Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB Window) na dola za Marekani milioni 42 zitatolewa kupitia mfuko wa Africa Growing Together Fund (Mfuko wa Serikali ya China unaosimamiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika)” alisisitiza Bw. James.

Aliishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za uwekezaji katika miundombinu ya usafiri itakayoiwezesha Tanzania kufikia azma yake ya kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.

“Uwekaji saini wa Mikataba hii miwili itaongeza kiasi cha fedha ambacho kimetengwa na Benki kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa barabara nchini Tanzania, kutoka dola za Marekani milioni 858.16 hadi dola za Marekani bilioni 1.038, sawa na takribani sh. trilioni 2.39”, aliongeza Bw. James.

Alisema Barabara hiyo inaungana na barabara ya Cape hadi Cairo inayojulikana kama the Great North Road Highway yenye urefu wa km 10,228 inayopita katika nchi nane ambazo ni Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Zambia, Tanzania, Kenya, Ethiopia, Sudan na Misri na ni barabara ya ukanda wa kati (central corridor) inayounganisha Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.

Alidokeza pia kuwa Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), imeonesha  utayari wa kufadhili ukarabati wa barabara ya Bagamoyo–Pangani-Tanga kwa kiwango cha lami na Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa-Msalato, utakaojengwa mkoani Dodoma  ambapo tayari maandalizi yameanza.

Kwa upande wake, Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), Bw. Alex Mubiru, alisema kukamilika kwa mradi huo kutaiunganisha Dodoma na mikoa mingine ikiwemo Arusha, Iringa, Singida, na Dar es salaam na kwamba utasaidia kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dodoma kwa sababu magari yanayokwenda kwenye maeneo hayo yatapita pembezoni mwa Jiji.

“Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na washirika wake tutatoa asilimia 84 ya gharama za mradi ambazo ni dola za Marekani Milioni 215 wakati Tanzania itatoa asilimia 16 na baadae mwaka huu tutatoa kiasi kingine cha msaada wa takriban dola milioni 7.2 ambazo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha mazingira kwa kupanda miti kwenye eneo la mradi” alisema Bw. Mubiru.

Aliongeza kuwa hivi sasa Benki yake inajiandaa kutoa mkopo kwa ajili ya miradi miwili muhimu ukiwemo mradi wa uboreshaji wa  barabara kutoka Bagamoyo-Pangani-Tanga-Horohoro/lunga, Lunga – Mombasa-Malindi pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa-Msalato, miradi ambayo Bodi ya Benki hiyo inatarajia kuipitisha mwishoni mwa mwaka 2019.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakibadilishana hati za mikataba ya mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshaji wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini-TANROADS, Mhandishi Patrick Mfugale, akiwaeleza wanahabari kuhusu michoro ya mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko katika Jiji la Dodoma ambao Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) umetoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya kuutekeleza katika kipindi cha miaka miwili ijayo.


Chanzo: thehabari.blogspot.com

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.