Na. Dennis Gondwe, DODOMA
SOKO la wazi la Machinga kuliingizia Jiji la Dodoma mapato ya shilingi 1,780,368,000 kwa mwaka yatakayosaidia kuboresha huduma za jamii.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jijila Dodoma, Joseph Mafuru alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka miwili Jijini Dodoma.
Mafuru alisema kuwa ujenzi wa Soko la wazi la Machinga katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma umegharimu kiasi cha shilingi 9,529,747,200.66. Fedha zilizotumika katika ujenzi wa Soko la wazi la Machinga, shilingi 6,529,747,200 ni mapato ya ndani ya halmashauri, shilingi 2,500,000,000 ni ruzuku kutoka serikali kuu na shilingi 500,000,000 ni fedha kutoka mapambano dhidi ya Uviko -19.Halmashauri ya Jiji la Dodoma tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha fedha katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa Sko lawazi la Machinga alisema Mkurugenzi Mafuru.
Akiongelea mchango wa soko hilo la wazi, alisema kuwa soko hilo limewawezesha wafanyabiashara wadogo kufanya biashara zao katika mazingira bora na yenye staha. Alisema kuwa halmashauri inatarajia kukusanya shilingi1,780,368,000 kwa mwaka kutokana na maeneo ya kibiashara katika soko hilo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.