MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi ametoa wito kwa waandaaji wa vyakula hususan katika ngazi ya Kaya wakiwemo akina mama katika Halmashauri hiyo kuimarisha na kuzingatia usafi wakati wa uandaaji kwani zaidi ya asilimia 70 ya maradhi katika jamii yanasababishwa na uchafu.
Kunambi alitoa wito huo katika hafla ya kilele cha kampeni yaujenzi wa Vyoo bora katika Halmashauri hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mnadani Jiji humo, ikiwa na kauli mbiu isemayo “Usichukulie poa,Nyumba ni Choo.”
Ofisa Afya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Abdallah Mahia akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi huyo alisema akina Mama wana nafasi kubwa ya kuzuia Magonjwa hususan ya tumbo ikiwa watalipa kipaumbele suala la usafi ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kila wanapotoka chooni, huku akisisitiza ujenzi wa Choo bora kwa kila Kaya.
“Akina Mama ndiyo mnaotuandalia chakula, kama hutazingatia unawaji wa mikono baada ya kutoka chooni basi familia yako utailisha uchafu”alisema Kunambi.
Kwa upande wake, Afisa Afya wa Halmashauri hiyo Abdallah Mahia alisema mpaka sasa asilimia 97.38 ya Kaya zina Vyoo bora, na kwamba kampeni hiyo ililenga kuhamasisha jamii kujenga na kutumia Vyoo Bora kupitia Kampeni ya Taifa ya usafi inayoratibiwa na Wizara ya Afya.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.