Na. Shaban Ally, Dodoma
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ikiongozwa na mwenyekiti wake, Murshid Ngeze aipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kutekeleza mradi mkubwa wa kimkakati wa soko la kuu la machinga.
Pongezi hizo alizitoa alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo ambapo aliongozana na uongozi wa halmashauri hiyo pamoja na wajumbe wa ALAT Taifa.
Ngeze alipata wasaa wa kuzungumzia jinsi alivyovutiwa na ujenzi huo wa soko la machinga ambao umegharimu mabilioni ya fedha ambazo kwa kiasi kikubwa umejengwa kupitia mapato ya ndani yanayokusanywa na Halmashauri ya jiji hilo. Ambapo kwa kiasi kikubwa mwenyekiti alitumia fursa hiyo kutoa pongezi zake za dhati kwa mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Joseph Mafuru pamoja na mkuu wa mkoa, Anthony Mtaka kwa kufanya Dodoma izidi kung'ara.
"Kwa niaba ya ALAT, nikushukuru sana mkuu wa wilaya pamoja na viongozi wengine wa jiji kwa kuupiga mwingi. Lakini nikuombe mheshimiwa mkuu wa mkoa kuzingatia suala la usalama katika eneo hili la mradi ili kuepusha usumbufu kwa wafanyabiashara",alisema Ngeze.
Sanjari na hilo, mwenyekiti huyo wa ALAT aliendelea kutoa ushauri kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuzingatia maendeleo ya kiuchumi kwa wafanyabiashara hao kwa kuwapa elimu ya biashara ili kuweza kuwakomboa kiuchumi.
"Nikuombe mheshimiwa mkuu wa mkoa uweke utaratibu wa mafunzo ya biashara kwa wafanyabiashara hao kwa lengo la kumuendeleza mfanyabiashara huyo",aliongeza Ngeze.
Mwenyekiti huyo wa ALAT, Murshid Ngeze alihitimisha kwa kuwaomba viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma hususani wajumbe wa ALAT kwenda kujifunza miradi ya maendeleo katika Halmashauri yake ya Kagera, ambapo hii itapanua mawazo ya kimaendeleo kwa viongozi hao.
Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago alipata fursa ya kutoa maneno machache kuhusu ukuaji wa kasi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambapo alianza kwa kumpongeza mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia halmashauri hiyo kiasi cha fedha kwa lengo la kumalizia mradi wa soko la machinga.
Chibago aliendelea kueleza jinsi Halmashauri ya Jiji la Dodoma linavyopokea wageni kutoka halmashauri nyingine kuja kujifunza kuhusu utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimakakati ambayo kwa kiasi kikubwa huchangia kiasi kikubwa cha mapato Katika halmashauri.
Aidha, naibu meya huyo, alihitimisha kwa kuwaomba viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na wale wa ALAT kudumisha umoja na ushirikiano baina yao ili kuchochea maendeleo zaidi.
"Niwaombe ndugu viongozi wenzangu kwa pamoja tudumishe umoja wetu na ushirikiano kwa kuwa asije akatokea mtu yeyote wa kuvunja umoja wetu",alisema Chibago.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka mbele ya wajumbe wa ALAT Taifa akielezea jinsi mkoa wake ulivyojipanga kuzisimamia Halmashauri zake katika kutekeleza miradi ya maendeleo yenye tija kwa wananchi wa mkoa huo.Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri akiongea mbele ya wajumbe wa ALAT Taifa walipotembelea jiji la Dodoma lililopo ndani ya Wilaya ya Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru akiongea mbele ya wajumbe wa ALAT Taifa jinsi jiji hilo lilivyojipanga kuhakikisha miradi mikubwa ya kimkakati inavyosimamiwa na kutekelezwa ili kuwa na tija kwa wananchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.