Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Kamati ya Ushauri Wafanyakazi Wanawake ya TALGWU Mkoa wa Dodoma, imetembelea Kituo cha Afya Mkonze katika kufanya matendo ya huruma na kukabidhi msaada wa tenki la maji lenye ujazo wa lita 4,000.
Akizungumza na uongozi wa Kituo cha Afya Mkonze, Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri Wafanyakazi Wanawake ya TALGWU Dodoma, Siwajibu Clavery alisema, “maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yana dhima kubwa sana hasa ukizingatia mwanamke ndio kinara wa majukumu kwenye sehemu muhimu za familia. Sisi tumeona ni vema kufanya matendo ya huruma na kutoa msaada wa tenki hili ili wagonjwa hasa wanawake waweze kupata huduma ya maji wawapo katika matibabu kituoni hapa. Tunaomba mtumie kwa lengo hili kusudiwa”.
Nae Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mkonze, Halima Kheri alisema anashukuru sana kwa msaada huo na atahakikisha linatumika vema ili huduma ya maji ya ziada kituoni hapo isikosekane.
Msaada huo wa tenki la kuhifadhia maji limegharimu kiasi cha shilingi 800,000 wakiwa na matajario ya kupunguza adha ya maji katika Kituo cha Afya Mkonze.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.