WAFANYABIASHARA na Wawekezaji kutoka Jiji la Linz nchini Austria wamealikwa kuwekeza katika kilimo cha zao la Zabibu ili kukuza uchumi wa Wananchi wa Jiji la Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Mshahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe. Prof. Davis Mwamfupe alipokuwa akiwatembeza wageni kutoka jiji la Linz la nchini Austria katika shamba la Zabibu lililopo eneo la Mpunguzi kata ya Matumbulu Jijini humo.
Meya Mwamfupe alisema kuwa zao la Zabibu ni nembo na ‘Tanzanite’ ya Dodoma na kwamba changamoto kubwa ni kilimo cha kisasa na soko la zao hilo.
Aidha, aliwataarifu wageni hao walioongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Linz Klaus Luger kuwa wanakaribishwa kuwekeza katika kilimo cha zabibu na soko la zao hilo.
Timu ya wageni nane kutoka jiji la Linz nchini Austria wakiongozwa na Mstahiki Meya Klaus Luger wapo katika ziara ya siku mbili katika Jiji rafiki la Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine, pande hizo mbili zitasaini hati ya makubaliano ya ushirikiano pamoja na kukabidhi gari la Zimamoto kwa Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.