Asasi za kiraia zimetakiwa kuhakikisha shughuli wanazofanya zinalenga kuwanufaisha wananchi hadi ngazi ya chini.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito huo akifungua Kongamano la kwanza la Asasi za Kiraia (AZAKi) za Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, jijini Arusha .
Dkt. Gwajima alibainisha kuwa, ushiriki wa watu kupitia AZAKi ni muhimu kuhakikisha sera zinafanya kazi hadi mashinani na nafasi muhimu ya Asasi za Kiraia kwenye utafiti, mijadala na kufanya mikutano ya hadhara kuhusu masuala muhimu kwa wananchi.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kukuza ushirikiano na asasi zisizo za kiserikali ili kutunga sera zinazonzingatia mahitaji ya watu na kukuza ukuaji wa uchumi wa jamii ndadani ya kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki". alisema Dkt. Gwtajima na kuongeza kuwa. "Ni matumaini ya Serikali kuwa, mkutano huu utaandaa viashiria vya wazi vya ushirikishwaji ili kuhakikisha ushiriki mahiri wa AZAKi kama sauti ya wananchi katika ngazi ya kikanda". Alifafanua Waziri Dkt. Gwajima.
Dkt. Gwajima aliongeza kwamba, licha ya mambo mbalimbali ya AZAKi ndani ya nchi washirika, jumuiya imeendelea kuhamasisha ushiriki wa Asasi za kiraia na jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuhakikisha sauti za wananchi wa Afrika Mashariki zinawasilishwa na kuzingatiwa wakati wa kufanya maamuzi.
Aidha, alisema anaamini Mkutano huo utawezesha AZAKi kuonesha mafanikio na programu zenye matokeo katika kanda na kuja na matarajio ya wananchi kwa kujikita kwenye mada kama vile za Afya, Utawala na Demokrasia, Biashara na Uwekezaji, Amani na Usalama, Kilimo, Mabadiliko ya Tabianchi, ushiriki wa Jinsia na Vijana ili kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kijamii na kukuza ustawi wa raia.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.