MPANGO na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma umepongezwa kuwa ni mzuri na unakwenda kuwahakikishia wananchi huduma bora za kijamii.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Zuzu, Awadhi Abdallah alipokuwa akichambua Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma baada ya kupitishwa na mkutano wa Baraza la Madiwani.
Abdallah alisema kuwa Mpango na Bajeti hiyo ni nzuri kuliko zote. “Halmashauri ya Jiji imekuwa ikifanya mambo mazuri lakini bajeti ya safari hii imejikita kufanya mambo mazuri zaidi. Bajeti inagusa maeneo mengi ya jamii na mtu mmoja mmoja kuhakikisha huduma bora inamfikia kwa ukaribu mno” alisema Abdallah.
Alisema kuwa madiwani na wataalam wanawajibu wa kuhakikisha mapato yanakusanywa kikamilifu. “Tunawajibu wa kuzuia uvujaji wa mapato na kuhakikisha fedha hizo zinakwenda kutumika kikamilifu chini ya usimamizi wa ngazi ya Halmashauri nasisi viongozi wa ngazi ya kata na mitaa” alisema Abdallah.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lilipitisha makisio ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya shilingi 128,278,555,369. Kati ya fedha hizo, shilingi 55,128,229,369 ni mapato ya ndani na shilingi 59,082,835,000 ni ruzuku ya mishahara. Ruzuku ya matumizi mengineyo ni shilingi 1,005,792,000 na shilingi 13,061,699,000 ni ruzuku ya miradi ya maendeleo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.