HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kupandisha makisio ya bajeti kutoka shilingi bilioni 3.9 mwaka wa fedha 2016/2017 hadi kufikia shilingi bilioni 67 mwaka wa fedha 2018/2019 na kuongeza wigo wa kutoa huduma kwa wananchi wake.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alipokuwa akiwasilisha maelezo mafupi juu ya utekelezaji wa majukumu ya Jiji la Dodoma kwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma mjini Mhe. Josephat Maganga leo.
Kunambi amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa mapato na usafi wa mazingira. “Mwaka 2016/2017 Halmashauri ilipanga kukusanya shilingi bilioni 3.9 za mapato ya ndani ya Halmashauri, lakini tukakusanya shilingi bilioni 4.3. Mwaka 2018/2019, makisio ya bajeti yalipanda kutoka shilingi bilioni 20 hadi kufikia shilingi bilioni 67”. Alisema kuwa kuongezeka kwa mapato ya ndani ya Halmashauri kumeiwezesha Halmashauri ya Jiji kutekeleza majukumu yake mengi ya kuhudumia wananchi katika nyanja za elimu, afya, usafi wa mazingira, ardhi na mipango miji.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma amefanya ziara ya kawaida katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kujitambulisha pamoja na kuongea na timu ya Menejimenti ya Halmashauri.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Josephat Maganga akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi mbele ya timu ya menejimenti ya jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.