Watanzania 4,247 wamepata fursa ya kusoma Shahada ya Uzamili na Uzamivu nchini China katika kipindi cha miaka mitano iliyopita iliyowapatia ujuzi utakaotoa mchango wa ujenzi wa taifa katika fani mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki alipokuwa akielezea mafanikio ya Mhula wa Kwanza wa Serikali ya Awamu ya Tano katika mahusiano ya kidiplomasia na nchi hiyo.
Amesema kuwa matarajio kwa miaka mitano ijayo ni kufungua fursa zaidi ili watanzania wengi waweze kusoma nchini humo kwa lengo la kuwaongezea ujuzi.
Aidha, Balozi Kairuki amebainisha kuwa katika masuala ya afya uhusiano baina ya nchi hizo mbili umewezesha wataalamu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kufika katika hospitali ya FUWAI nchini China kufanya mafunzo ya vitendo.
Katika hatua nyingine, Balozi Kairuki amesema kuwa soko la wafanyabiashara wa kitanzania nchini China limefikia dola milioni 145, kwa miaka mitano iliyopita.
Chanzo: HabariLeo
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.