Na Angela Msimbira, UGANDA
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Simuli ametoa rai kwa vijana wote nchini Tanzania kushiriki michezo ili kupata ajira na kujenga mahusiano na nchi nyingine.
Akizungumza na wachezaji wa Tanzania wanaoshiriki Mashindano ya 22 ya michezo ya shule za Msingi na Sekondari ya Nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki (FEASSSA) yanayofanyika nchini Uganda, Balozi Simuli amesema pamoja na michezo kujenga afya lakini inatoa fursa ya ajira kwa vijana.
"Mmekuja kwenye mashindano haya ni muhimu yanawapa furaha na kuwaunganisha pamoja vijana wa Afrika Mashariki. Viongozi mtoe kipaumbele kwenye michezo ili tupate vijana mahiri kwa kuwa ni eneo pia linalotoa ajira kwa vijana," amesema.
Amewataka vijana wa Tanzania kujitokeza kwenye michezo kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi kwenye michezo hivyo ni jukumu la watanzania kuonyesha vipaji vyao na kuleta ushindi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.