HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inatekeleza mpango wa uchongaji wa barabara mpya za mitaa katika eneo la Mtumba ili kuruhusu miundombinu mingine ya maji na umeme kuanza kuwekwa na kuandaa mazingira mazuri kwa wamiliki wa viwanja kuanza ujenzi.
Eneo hili linapakana na mji wa serikali kwa kutenganishwa na barabara kuu ya Dar es Salaam ambapo Umilikishwaji wa viwanja zaidi ya elfu 11 umekamilika na maandalizi ya nyaraka za umiliki yanaendelea.
"Kwa mujibu wa mkataba kazi hii inatakiwa ikamilike ndani ya siku 90 lakini tumewasisitiza kampuni ya Yakil Investiment Ltd wakamilishe mapema ili tusiwacheleweshe wananchi kufanya uendelezaji wa maeneo yao." alisema Joseph Mafuru, Mkuu wa Idara ya Ardhi, Mipango Miji na Maliasili jiji la Dodoma.
Jumla ya kilomita 375 za barabara zinatarajiwa kuchongwa katika eneo hili na tayari kampuni ya Yakil Investment Ltd imeshakamilisha kuchonga umbali wa kilomita 50.
Naye Msimamizi wa kampuni ya Yakil Ivestment Mhandisi Daudi Ibrahim amesema mitambo miwili ya uchongaji wa barabara hizo ipo katika eneo hilo na wanataraji kuongeza mitambo mingine ili kuharakisha ukamilishaji wa kazi hiyo mapema kabla ya muda uliopangwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.