Ujenzi wa Barabara ya kilometa 5.2 inayounganisha Kata ya Dodoma Makulu na Ntyuka kutatua changamoto ya usafi kwa kata hizo na kufanya maisha ya wananchi kuwa bora.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Msangalale Magharibi Kata ya Dodoma Makulu, Leonard Ndama alipokuwa akiongelea mchango wa Barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 5.2 katika mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka minne.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka minne ilianza ujenzi wa barabara yenye kiwango cha lami iliyokuwa ni changamoto kwa wakazi wa Kata ya Dodoma Makulu walipotaka kwenda Ntyuka kufuata huduma za kijamii. Alisema kuwa walikuwa wakitumia muda mrefu njiani na kuchelewa shughuli zao jambo lililosababisha uchumi wao kuwa chini.
“Tumepata mradi huu wa barabara inayotoka Dodoma Makulu kwenda Ntyuka ambayo imeleta manufaa ya kibiashara hata katika usafiri kwasababu wananchi wamekuwa wakitumia barabara hii. Naomba wananchi wa Dodoma Makulu tuitunze miundombinu hii tuliyojengewa na serikali ili tuweze kurithisha vizazi vyetu vijavyo” alisema Ndama.
Nae, mwananchi wa Kata ya Dodoma Makulu, Nazarius Moshi anayejishughulisha na biashara ya usafirishaji maarufu kama bodaboda, alieleza namna barabara hiyo itakavyoleta faida kwa watumiaji wa barabara hiyo itakapo kamilika hasa wafanya biashara ya usafirishaji (bodaboda). “Barabara hii ikikamilika itakuwa na faida kwetu kwasababu kwanza, itaturahisishia katika shughuli zetu za usafirishaji wa abiria kutoka Kata ya Ntyuka, zamani tulikuwa tunateseka sana na ubovu wa barabara hii. Pili, itarahisisha wananchi kuzifikia huduma za kijamii nje ya kata hii kwa urahisi” alisema Moshi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.