BARAZA la Maadili lipo kwenye uchunguzi wa Malalamiko tisa toka sehemu mbalimbali, uchunguzi huo umeanza Septemba 6 na utatamatika Septemba 16 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Kamishina wa Maadili, Jaji Sivangilwa Mwangesi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Mwangesi amesema kamishina wa maadili ndiye anayepokea malalamiko toka sehemu tofauti tofauti na kuaza uchunguzi wa malalamiko hayo na baadae kuwakilisha malalamiko hayo kwenye baraza la maadili.
" Mpaka sasa kuna malalamiko tisa ambayo yanachunguzwa na baraza la maadili baada ya uchunguzi huo baraza litaandaa maoni yake kutokana na lalamiko lililotolewa na ushahidi ambao umepokelewa, uchunguzi huu unafanyika kwa mujibu wa kifungu cha 25(5) na 296 cha Sheria ya Maadili ya Uongozi wa Umma ( sura 398)" amesema Mwangesi.
Pia amesema baraza halitakuwa na siku ya kutoa hukumu bali litachukua uamuzi wake kulingana na sheria ilivyo na litatoa ushauri baada ya hapo anakabidhiwa kamishina wa maadili kwa ajili ya kupeleka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema jukumu kubwa la Taasisi hiyo ni kuchunguza tabia ya mwenendo wa kiongozi wa umma yoyote kwa madhumuni ya kuhakikisha masharti ya sheria ya maadili ya uongozi wa umma yanazingatiwa .
Chanzo: Michuzi Blog
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.