Na. Coletha Charles, DODOMA
Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Jiji la Dodoma limefanya kikao maalum kwa ajili ya kupitia bajeti ya mpango wa makisio ya mapato na matumizi ya mwaka 2025/2026, ambayo imeongezeka kwa asilimia 7.04 ukilinganisha na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Kikao hiko kilifanyika katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri Jiji hilo, ambacho kililenga mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia miongozo ya dira ya maendeleo ya taifa 2025, mpango wa maendeleo wa miaka 5, sheria ya bajeti na. 11 ya mwaka 2015 na malengo endelevu ya maendekeo (SDGs).
Akiwasilisha rasimu ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Francis Kaunda, alibainisha kuwa halmashauri ipo kwenye kundi la utengaji wa fedha kwa asilimia 70 ya mapato yasiyolindwa kwenda kwenye miradi ya maendeleo na asilimia 30 kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Alisema kuwa miradi ya maendeleo 70% sawa na shilingi bilioni 30.1, matumizi ya kawaida 30% sawa na shilingi 12.9, wanawake, vijana na watu wenye ulemavu 10% shilingi bilioni 4.3, barabara 10% shilingi bilioni 4.3, miradi viporo shilingi bilioni 7, miradi mikakati shilingi bilioni 5, miradi ya kipekee shilingi bilioni 1, miradi ya kata shilingi bilioni 6.1 na vipaumbele vingine vya divisheni shilingi 2.3.
“Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji, naomba kutamka rasmi kuwa rasimu ya makisio ya mpango na bajeti ya Halmshauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2025/26 ni jumla ya shilingi bilioni 147.9, kati ya fedha hizo shilingi bilioni 67.3 ni mapato ya ndani, shilingi bilioni 65.7 ruzuku ya mishahara, shilingi bilioni 3 ruzuku ya matumizi mengineyo na shilingi bilioni 11.7 ruzuku ya miradi ya maendeleo”.
Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, pia aliwasilisha mapitio ya bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2024/25, ambapo alisema Halmshauri ya Jiji la Dodoma iliidhinishiwa bajeti ya shilingi bilioni 143.1 hadi kufikia desemba 2024, jumla ya shilingi bilioni 76.1 zilikusanywa sawa na 53.2% ya makisio.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.