BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limepitisha mpango na bajeti ya shilingi 120,841,764,871 ya Halmashauri hiyo kwa ajili shughuli za mbalimbali katika mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwemo miradi ya maendeleo na masuala ya utawala na uendeshaji wa Halmashauri hiyo.
Bajeti hiyo imepitishwa na mkutano maalum wa Baraza hilo leo Machi 10, 2021 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo kikiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe na Katibu wake ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji Joseph Mafuru.
Akiwasilisha Mpango na Bajeti hiyo mbele ya Baraza, Katibu ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji Mafuru alisema kuwa fedha hizo zinatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo vya ndani, Serikali Kuu, na Wahisani mbalimbali, ambapo zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo, utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii, pamoja na masuala ya utawala na uendeshaji wa Halmashauri.
Mafuru alisema bajeti ni rafiki kwa wakazi wa Jiji la Dodoma kwani asilimia 83 ya fedha hizo itaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na huduma mbalimbali za kijamii.
Baraza hilo kwa kauli moja moja lilipitisha bajeti hiyo huku wajumbe wakitoa pongezi kwa wataalam wa Halmashauri kwa kuandaa bajeti yenye uhalisia na iliyolenga kuboresha maisha ya wakazi wa Dodoma kwa miradi na huduma zingine kama elimu afya na miundombinu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.