WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo amezungumza na Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Maafisa biashara wa Mikoa, Mawakala wa saruji walioko mikoani na wakurugenzi wa viwanda vya saruji.
Katika mkutano huo Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara ikamilishe utaratibu wa kuwa na bei kikomo ya saruji ili kuuwezesha kila mkoa kujua bidhaa hiyo inapaswa kuuzwa kwa bei gani kwa ania ya kuondoa upandishwaji holela unaofanywa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka Mawakala wabadilike na waachane na tabia ya kuficha bidhaa kwa ajili ya kuzipandisha bei, kwani mtu yeyote akikutwa anatengeneza mazingira ya kufanya bidhaa isipatikane kwa lengo la kupandisha bei huo ni uhujumu uchumi na ikiwa atakutwa na bidhaa ambayo inatafutwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.