TIMU ya maafisa kutoka Benki ya Dunia wamefanya ziara ya kukagua mradi wa dampo la kisasa na Barabara zinazofadhiliwa na Benki hiyo katika Manispaa ya Dodoma chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Miji Tanzania (TSCP).
Ziara hiyo ilifanyika jana April 6, 2017 ambapo timu hiyo ilitembelea eneo la Chidaya unakotekelezwa mradi wa dampo la kisasa linalotumia teknolojia ya kuzika taka (Land Fill) na kufurahishwa na maendeleo ya mradi ambao umeashaanza kufanya kazi huku ujenzi ukiwa katika hatua za mwisho.
Aidha ujumbe huo ulitembelea barabara zilizojengwa chini ya mradi huo unaotekelezwa katika Manispaa Saba Tanzania Bara pamoja na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA).
Awali ujumbe huo ulikutana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi na kufanya nae mazungumzo mafupi, ambapo aliishukuru Benki ya Dunia kwa kusaidia kuboresha miundombinu katika Manispaa ya Dodoma huku akiiomba kuendelea kutoa ufadhili zaidi ili kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kisasa zaidi hivyo kuendana na hadhi yake ya kuwa makao makuu ya Nchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.