Ujumbe kutoka Benki ya Dunia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI anayeshughulika na masuala ya Afya Dkt. Zainab Chaula wameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa usimamizi bora wa majengo mapya ya upanuzi wa Kituo cha Afya Makole yaliyojengwa kwa ufadhili wa benki hiyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuongeza fedha kiasi cha shilingi milioni 72 kukarabati majengo ya zamani ili yaendane na mandhari ya majengo mapya.
Katika mazungumzo yaliyofanyika Kituo cha Afya Makole, Mganga Mkuu wa Jiji Daktari Gatete Mahava ameshauri kujengwa kwa ukuta upande wa mashariki mwa kituo hicho ili kuongeza utulivu na usiri kwa wagonjwa.
Aidha, Daktari Mahava amependekeza ujenzi wa majengo ya kwenda juu (ghorofa) kwenye eneo lililokuwa na nyumba ya mtumishi pamoja na ujenzi wa kantini ndogo kwa ajili ya huduma ya chakula.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI - Afya pamoja na ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia wameahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yote ili kuboresha huduma katika kituo hicho.
Mbali na kituo cha Afya Makole, wageni hao walitembelea vituo vya Afya vilivyoko katika Halmashauri ya Kongwa na Chamwino.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.