Mratibu wa Mradi wa Uendelevu wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSS) kutoka TAMISEMI Bw. Seleman Yondu amesema mradi huo ukwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 umepokea jumla ya Tsh. 83.1Bil kwa ajili ya utekelezaji wake huku eneo la Afya ikitumia shilingi Bil. 54.39 na ujenzi wa miundombinu ya Elimu ikitumia shilingi Bil. 28.73
Amesema, Mradi unatekelezwa katika mikoa yote 25 ya Tanzania bara na Halmashauri 137, huku akiweka bayana kuwa Manispaa, miji na majiji sio sehemu ya mradi huu.
Yondu ameyasema hayo Julai 17,2024 wakati wa kikao kazi kilichofanyika mkoani Morogoro kikiwahusisha waganga Wakuu wa Mikoa na Maafisa Afya wa Mikoa yote Tanzania Bara lengo likiwa ni kujitathmini juu ya utekelezaji wa Mradi huo.
Amesema mpaka sasa mradi wa SRWSS umefikia vituo vya kutolea huduma za Afya 2,727 na shule za Msingi 1,842, kwa mwaka wa fedha 2023/24 jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 838 na shule 566 vimepokea fedha za utekelezaji.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Anyantike Mwakitalima amesema mradi huo umefanyika kwa mafanikio hususan ukilinganisha malengo na kazi iliyofanyika huku akibainisha kigezo kimojawapo kuwa kaya zenye watu zaidi ya 10,000zimefikiwa na kutoa elimu ya kuwa na vyoo bora na kuvitumia huku lengo likiwa ni kuzifikia kaya zenye watu 9,000.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Best Magoma ameishukuru Serikali kwa kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za Afya ameiomba Serikali usafiri wa pikipiki kwa ajili ya watendaji wakutoa huduma za Afya ngazi ya chini ili kuwawezesha watendaji hao kufika kila kaya na kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Naye Afisa Afya Mkoa wa Morogoro Bi. Prisca Laurent kwa niaba ya washiriki wengine amesema kufanya vizuri katika mradi huo utapunguza magonjwa ya mlipuko lakini pia kuziwezesha Halmashauri kupewa fedha zaidi.
Aidha, amebainisha kuwa uhamasishaji wa kujenga na kutumia vyoo bora kwa wananchi wa Mkoa huo umeongezeka kutoka asilimia 72 hadi 73 na kwamba Mkoa huo kuanzia mwaka 2023 tayari umepokea zaidi ya Tsh. 3 Bil. Kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.