SERIKALI ya awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Bilioni 3.4 kwa dhumuni la kulipa fidia wananchi wa Jiji la Dodoma ambao ardhi zao zilitwaliwa kwa matumizi mbalimbali ya Serikali.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa zoezi la ulipaji wa fidia ya ardhi iliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mbabala iliyopo jijini hapo.
Senyamule alisema kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani na utulivu, kwa kuhakikisha wanatatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kero za ardhi.
“Leo nakabidhi mfano wa hundi yenye jumla ya shilingi 3,068,705,727.81 zitakazolipwa kwa wananchi 314, malipo hayo yatafanyika mara baada ya uhakiki wa uhalali wa fidia, timu ya uhakiki tayari imeshaundwa na imeshaanza kufanya kazi yake.Katika uhakiki wa awamu ya kwanza jumla ya wananchi 127 wamekidhi vigezo na wanalipwa jumla ya madai ya shilingi 1,735,901,727.81.
Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj. Jabir Shekimweri amewasihi wananchi ambao hawajajitokeza kuhakikiwa viwanja vyao, wajitokeza ili waweze kulipwa madai yao. “Niwaombe wananchi wote ambao wanamadai ya fidia ya ardhi wajitokeze ili kufanyiwa uhakiki wa uhalali wa madai yao, wale waliokidhi vigezo waweze kulipwa fidia kwa mujibu wa makubaliano yao na Serikali. Lengo letu ni kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Dodoma hawalii kutokana na changamoto ya ardhi, na hiyo ndio dira ya serikali yetu kuhakikisha inatatua changamoto za wananchi” alisema Alhaj Shekimweri.
Miongoni mwa kata zinazonufaika na fidia hizo ni pamoja na Iyumbu, Chigongwe, Mbalawala, Makole, Zuzu, Kikombe, Mtumba, Chahwa, Miyuji na Mlimwa C ambazo zote zinapatikana ndani ya Wilaya ya Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.