HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma leo Jumanne Juni 26, 2018 imesaini mikataba mitatu ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika jiji hilo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 77.8, katika hafla ya utiaji saini iliyohudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo katika viwanja vya Nyerere jijini humo.
Miradi inayotarajiwa kujengwa na kubadili muonekano wa Jiji la Dodoma ni pamoja na Stendi Kuu ya kisasa ya Mabasi, Soko Kuu la kisasa, Barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 26.62, Pea 7 za vizimba vya kukusanyia taka, Kituo kikuu cha kuegesha malori, Bustani ya kupumzikia yenye viwanja vya michezo mbalimbali, Taa 913 katika mitaa mbalimbali, Vivuko 6 vya waenda kwa miguu, na mitaro ya maji ya mvua yenye urefu wa kilometa 6.5.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Jafo aliwatahadharisha Makandarasi na Mhandisi Mshauri kutoharibu miradi hiyo na kuwataka kukamilisha kwa wakati, ambapo Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi alisema miradi yote hii itajengwa na Makandarasi watatu tofauti kuanzia Julai Mosi, 2018 na inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 15 ijayo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.