Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Mkoani Dodoma (Dodoma Youth Development Organization - DOYODO) kupitia Mradi wa Uraghibishi wa Magauni Manne imewakutanisha walimu wa Shule za msingi na sekondari na Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata wa Jiji la Dodoma na kufanya kikao kazi.
Lengo la kikao kazi hicho kilichofanyia tarehe 29/08/2019 katika ukumbi wa mikutano wa Jiji la Dodoma ilikuwa ni kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na tatizo la mimba za utotoni. Kwa msisitizo kuwa Dodoma bila mimba za utotoni inawezekana kila mmoja akichukua na kutekeleza jukumu lake.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Afisa Afya na Katibu wa Afya wa Jiji ambao walipata fursa ya kuzungumza na wajumbe hao juu ya mipango na mbinu za kupambana na mimba za utotoni kuhakikisha mimba kwa wanafunzi mashuleni zinakomeshwa.
Naye Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Dodoma Sharifa Nabalang'anya aliyekuwa miongoni mwa watoa mada aliipongeza taasisi ya DOYODO na kusema "kazi yenu ni nzuri na ni sehemu ya kazi zangu, hivyo tutaendelea kushirikiana kwa kila hali". Alisema jamii nzima inatakiwa kushiriki katika zoezi hili litakalookoa vijana wengi wa kike wanaorubuniwa na watu waharibifu katika jamii yetu.
Aidha mmoja wa wanachama wa DOYODO Adam Cosmas, alimshukuru Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji Bi. Nabalang'anya na kusema "...hakika tunajivunia ushirikiano unaotupatia vijana wa DOYODO"
Kauli mbiu ya mkakati huu wa kumkomboa kijana wa kike ni "Binti tambua thamani yako, timiza malengo yako"
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Dodoma Sharifa Nabalang'anya akiongea na wadau wa mkakati wa kutokomeza mimba za utotoni (hawapo pichani). Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Mkoani Dodoma (DOYODO) Rajabu Nnunga.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.