WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri zote nchini kupitia Maafisa Michezo na Utamaduni kuandaa vikundi na viwanja kwa ajili ya kufanya mazoezi ili kuwajengea wananchi utamaduni wa kufanya mazoezi kuimarisha afya.
Waziri huyo amesema hayo jana jijini hapa katika Bonanza liloandaliwa na Benki ya CRDB, katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, huku akisema kila mtanzania anawajibu wa kufanya mazoezi kwa sababu ni afya.
Alisema, Halmashauri zinapaswa kuandaa viwanja kwa ajili ya kufanya mazoezi, hali itakayosaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha afya.
"Rais Samia katika moja ya hotuba zake alituasa tukitaka kwenda haraka twende peke yetu, lakini tukitaka kwenda mbali twenda pamoja,hivyo ni lazima tushirikiane kwa hili ili tufanikiwe zaidi,"alisema.
Waziri Mkuu aliishukuru benki ya CRDB kwa kuonyesha mfano wa kutuleta pamoja Bunge, Wizara pamoja na Wananchi wote kupitia bonanza waliloandaa.
Alizitaka na taasisi nyengine za umma na binafsi kuiga mfano wa Benki ya CRDB kwa kuandaa mabonanza kama hilo ilikuendelea kujenga utamaduni wa michezo na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Naye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dkt. Tulia Ackson aliiomba Benki ya CRDB kuendeleza utamaduni huo ambao wamekuwa nao kila mwaka Wa kushirikiana na Bunge katika kuhamasisha michezo na kujenga mahusiano.
“Tunawapongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa bonanza hili kwa mara nyengine tena, hii ni njia nzuri sana ya kujenga mahusiano huku tukiimarisha afya zetu,” amesema Dkt. Tulia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema lengo kuu la kuandaa bonanza hilo ni kuisogeza benki hiyo karibu na Serikali, Bunge na Wizara, ili kupata nafasi ya kusikiliza mahitaji yaliyopo na kujua namna gani benki hiyo inaweza shiriki kikamilifu katika mipango ya maendeleo ya nchi.
“Miaka ya nyuma tulikuwa tukifanya bonanza hili na Bunge, mwaka huu tumeshirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kushirikisha Wizara zote.
“Malengo yetu mwakani ni kuhusisha muhimili mwengine wa Serikali kwamaana ya Mahakama nao tuweze kushurikiana nao lengo ni kuongeza umoja na ushirikiano baina ya serikali na taasisi za fedha,” ameongezea Nsekela.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.