Bondia Hassan Mwakinyo amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Mabara wa uzito wa Super Welter wa WBF kwa kumsulubu kwa ‘Technical Knock Out’ (TKO) raundi ya nne bondia kutoka Argentina Jose Carlos Paz.
Akizungumza muda mfupi baada ya kutwaa ubingwa huo (13/11/2020), Mwakinyo alisema kuwa, kila anapomaliza pambano moja basi hufanya mazoezi mara mbili zaidi ya alivyojiandaa awali hivyo wapenzi wa ngumi wasitarajio kuone kiwango alichokionesha dhidi ya Paz katika pambano lijalo.
“Baada ya kushinda pambano hili nimepata nafasi ya kucheza ubingwa wa WBF, nitashinda kwa mara nyingine tena kupitia kwa kocha wangu huyu huyu ambaye watu walikuwa kimbeza kuwa si kocha mzuri,” alisema Mwakinyo.
“Mimi sio ‘boxer’ wa kufananisha na yeyote hapa nchini na nadhani kiwango nilichokionesha kimedhihirisha hilo kwani mara zote nawaambia mashabiki wangu kuwa mechi zinakuwa ngumu kulingana na ugumu na wapinzani na udhaifu wa elimu kwa makocha wetu hivyo wale waliokuwa wananitaja taja nadhani leo itakuwa mwisho wao kuongea kwani mimi ndio Tanzania One,” amesema Mwakinyo
Ikumbukwe kuwa Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni mwezi Februari 2021 kuzichapa na bondia Lasha Gurguliani kutoka Georgia.
Bondia Hassan Mwakinyo (kushoto) akimuadhibu bondia kutoka Argentina Jose Carlos Paz na kufanikiwa kuutetea ubingwa wake wa Mabara wa uzito wa Super Welter wa WBF.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.