NAIBU Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) ameyataka Mashirika ya Posta ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuchangamkia fursa za mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea duniani kwa sasa ili sekta hiyo iweze kutoa huduma bora zinazokidhi matakwa ya wateja.
Mhandisi kundo ameyasema hayo leo katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha, wakati akifungua Jukwaa la kwanza watoa uma wa Sekta ya Posta na Usafirishaji, lilioandaliwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki (EACO), huku likihusisha Mashirika yote ya Posta kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnaye(Mb), Mhandisi Kundo ameeleza kuwa jukwaa hilo lenye lengo la kuwakutanisha pamoja wadau wa sekta ya posta na kubadilishana uzoefu, waangalie namna bora zaidi ya kuboresha huduma za posta Kwa kuondoa changamoto ndogo ndogo zinazoikumba sekta ya Posta hasa baada ya utandawazi na teknolojia mpya na kujikita kwenye Biashara mtandao na huduma za fedha huduma jumuishi za kifedha kwa kufanya mabadiliko mahsusi ya kidijitali.
Mhandisi Kundo aliongeza kuwa, jukwaa hilo ni la kwanza kwa Mashirika ya Posta ya Jumuiya hiyo liwe chachu ya kutoa huduma huduma za posta zilizoboreshwa na kuwafikia wananchi wengi kwa haraka, ufanisi na kwa gharama nafuukupitia teknolojia za kisasa.
"Napenda kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri na rafiki sana ya kidiplomasia yanayotoa nafasi Kwa taasisi hizi kukutana Kwa uhuru na kujadiliana namna ya kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili watoa huduma mbalimbali katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hii inatokana na namna ambavyo Mh Rais Samia amekuwa kinara wa kuhakikisha mifumo na miundombinu ya mawasiliano nchini inazidi kurahisishwa na kuboreshwa kwa ajili ya maslahi ya wananchi" alisema Mhandisi Kundo
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.