Benki Kuu ya Tanzania (BOT), imesema imeandaa mfumo bora wa kuziwezesha taasisi binafsi na mashirika ya umma kuwekeza kwa faida badala ya kupata hasara katika shughuli za biashara na uwekezaji kwenye jamii.
Akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari za uchumi na biashara, Meneja wa Idara ya Masoko na Fedha wa BoT, Tawi la Arusha, Lameck Kakulu, alisema kuwekeza kuna faida kubwa kwa kuwa mwekezaji ana fursa ya kujipatia faida kuliko hasara.
Alisema kiwango cha riba kwenye dhamana za muda mfupi kilishuka kutoka asilimia 8.5 Agosti hadi asilimia 5.5 Desemba mwaka 2019.
Hata hivyo, alisema matokeo ya utekelezaji wa sera bora za fedha iliongeza ujuzi wa fedha kwenye benki kutoka wastani wa asilimia saba hadi nane.
Aidha, alisema benki za biashara ziliongoza ushiriki kwenye uwekezaji wa dhamana ya serikali kwa asilimia 67 na kwa upande wa mifuko ya pensheni, dhamana ilipanda kutoka asilimia nane hadi asilimia 20.
Pia alisema ushiriki wa wawekezaji binafsi dhamana ilipanda kutoka asilimia mbili hadi kufikia asilimia sita.
Aidha, alisema uwekezaji katika soko la upili zimeendelea kukua na dhamana ya muda mrefu imefikia thamani ya Sh. bilioni 815.70 na ziliuzwa na kununuliwa, ukilinganisha na kipindi kilichopita thamani hiyo ilikuwa Sh. bilioni 203.99.
Alisema ongezeko hilo lilitokana na kurejea sokoni kwa mifuko ya pensheni pamoja na kuongezeka kwa uelewa kwa wawekezaji wa mashirika na taasisi binafsi.
Kakulu alisema kiwango halisi cha dhamana za muda mfupi na muda mrefu kilichopatikana ni Sh. bilioni 2,572.52 sawa na asilimia 103, wakati kiwango kilichokusudiwa kiliongezeka kwa asilimia 42, ukilinganisha na mwaka wa 2018/19.
Kiwango kilichopatikana ni Sh. bilioni 1,192.69 na kiasi cha Sh. bilioni 1,379.38 zimetokana na dhamana za muda mfupi na mrefu.
Chanzo: www.ippmedia.com
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.