HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetenga Shilingi bilioni saba katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kujenga Jengo la Ofisi Kuu ya Jiji inayolingana na hadhi ya Makao makuu ya Serikali.
Jiji limetenga fedha hizo ambazo ni sehemu ya bajeti ya mwaka 2022/23 ya Shilingi bilioni 100.94 ambazo zitakusanywa na kutumika kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo huo wa ujenzi wa ofisi kuu ya Jiji hilo.
Akiwasilisha Bajeti ya Jiji kwa Mwaka 2022/23 mbele ya Baraza la Madiwani jijini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema Jiji limepanga kujenga ofisi bora itakayolingana na hadhi ya Jiji la Dodoma kama makao makuu ya serikali katika eneo la uwekezaji la Njedengwa na ujenzi wake utaanza Julai mwaka huu.
“Jengi la Makao Makuu ya Jiji litajengwa eneo la Njedengwa ambapo ni kati ya Jiji kwa sasa kwani jengo linalotumiwa kwa sasa lilijengwa na CDA mwaka 1973,” alisema.
Mafuru alisema pamoja na mradi huo, Jiji limeweka kipaumbele katika kukamilisha miradi viporo, kuchangia nguvu za wananchi, kujenga miradi ya maendeleo inayoleta tija, kuimarisha seka ya afya, elimu, kilimo na mifugo na kuimarisha utoaji wa huduma katika maeneo ya pembezoni.
Pia bajeti hiyo pia itazingatia stahiki za madiwani, stahiki za watumishi na mazingira mazufuri ya kufanyia kazi.
Akizungumzia bajeti ya mwaka uliotangulia kati ya kipindi cha Julai hadi Desemba alisema mwaka 2021, Shilingi bilioni 13.8 zimetumika katika kutekeleza miradi ya kimakati, upimaji wa ardhi, malipo ya fidia ya ardhi na miradi ya kijamii.
Pia imetumika katika kujenga mahakama ya jiji, ununuzi wa magari matatu kwa ajili ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato na ununuzi wa vifaa vya upimaji ardhi vilivyogharumi Sh milioni 240.
Pia halmashauri imefanikiwa kutoa mikopo kwa vikundi 49 yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.04 na kuendelea kukamilisha mradi wa kimkakati wa hoteli inayojulikana kama Dodoma City Hotel.
Pia kuendelea na ujenzi wa miradi ya kimkakati wa kitega uchumi katika mji wa Serikali Mtumba ambacho hadi sasa kimefikia asilimia 90 katika awamu yake ya kwanza.
Halmashauri pia imefanikiwa kufanya uthamini katika maeneo mbalimbali ya Nala, Mtumba, Kikombo na Ihumwa ambapo Shilingi bilioni 1.32 zimelipwa kama fidia kwa wananchi kupitia fedha za ndani.
Katika kipindi hicho Jiji limepima viwanja 10,339 katika maeneo mbalimbali ya Ngh’ongh’ona, Hombolo Bwawani, Zuzu na Mpunguzi. Pia limeandaa mipango 41 ya matumizi bora ya ardhi.
Katika kipindi cha Julai hadi Desemba, mwaka jana, Jiji hilo limetoa jumla ya hati 8,247 kwa wamiliki mbalimbali wa ardhi katika jiji hilo.
Pia limesimamia ujenzi wa madarasa 143 ya shule za sekondari na nne za msi ngi kupitia fedha za Covid-19 ambapo Sh bilioni 2.9 zilimtumika.
Lakini pia Jiji limekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 75 za vya shule za msingi na sekondaro kupitia fedha za ndani.
Katika bajeti ya mwaka 2022/23 Jiji linakusudia kukusanya na kutumia bajeti ya Shilingi bilioni 100.9, fedha hizo zitapatikana kupitia mkakati wake wa kukusanya madeni, kutumia vyanzo vya zamani na vipya kama minada.
Pia litahakikisha ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo na vituo vyote unatumia mfumo wa kielektroniki ili kuweza kudhibiti upotevu wa mapato hayo.
Pia Jiji katika kudhibiti makusanyo, linakusudia kuandaa kanzidata ya viwanja vyote vinavyozalishwa ili kudhibitiutoaji na ulipaji au uendeleaji wa viwanja hivyo.
Pia kufanya tathmini ya madeni ambayo halmashauri inadai tangu zamani hadi sasa ili kuhakikisha Jiji linaongeza mapato.
Linakusudia kuanzisha (SPV) ambayo itasimamia miradi yote ya kimkakati ikiwemo ya Hoteli ya Jiji Kitega Uchumi cha Halmashauri, Makazi ya Bei Nafuu, Soko Kuu la Job Ndugai, Kituo Kikuu cha Mabasi na Eneo la Kuegesha Maroli la Nala.
Pia litatumia watendaji wa kata, mitaa na vijana wanaoitwa Rangers pamoja na madiwani kufuatilia tozo, vibali vya ujenzi pamoja na leseni za makazi ili kuhakikisha kodi inakusanywa.
Akizungumza Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikira alisema ajeti inajitoshereleza na Mkurugenzi wa Jiji ametoa ufafanuzi kuhusu vifungu vyote hivyo wanaridhia kuipitisha.
Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe aliwahoji madiwani kuhusu bajeti hiyo ya 2022/23 na wakadhirika na kuipitisha kwa kauli moja na wakaahidi kwenda kusimamia makusanyo katika kata zao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.