Na. OR-TAMISEMI
SERIKALI imewataka Watendaji wa Sekta ya Elimu nchini kuacha visingizio wanapotekeleza majukumu yao bali watumie changamoto hizo kama fursa ya kuwaletea wananchi maendeleo na kuisaidia Serikali.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa mapema na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Dkt. Charles Msonde wakati akifungua kikao kazi cha nusu mwaka cha watekelezaji wa Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (GPE LANES II) kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Manispaa ya Morogoro.
Dkt. Msonde amesema kwa mtendaji yeyote changamoto lazima zitokee katika utekelezaji wa majukumu yake na hapo ndipo anatakiwa kuzitatua kwa wakati kwani fedha za miradi alizopewa zinatakiwa kutumika kwa wakati ili kutatua changamoto za kielimu zinazoikabili jamii.
“tuhakikishe kila mtu kwenye eneo lake anatimiza wajibu wake, simamieni vile mlivyopewa lakini ni lazima mshauri vizuri kitu kitokee” amesisitiza Dkt. Msonde.
Katika hatua nyingine Dkt. Msonde amesema Mradi wa GPE LANES II umefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Serikali na hivyo watendaji wahakikishe fedha zote za miradi zimetumika kabla ya tarehe 15, Januari, 2023.
“ni vizuri kuhakikisha kwamba fedha hizi zinapotolewa na Serikali ambazo ni masharti waliyokubaliana na Benki ya Dunia unatekeleza na kukamilisha miradi kwa mujibu wa masharti waliyoweka, fedha hizi zina deadline (ukomo wa matumizi) tarehe 15 Januari na haitakubalika na haikubaliki fedha yoyote ikafika tarehe 15 Januari” amesisitiza Dkt. Msonde.
Kwa upande wake Michael Ligola Mwenyekiti wa kikao kazi hicho ambaye pia ni Afisa Elimu Mkoa wa Songwe amesema kikao kazi hicho kina lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa kazi zilizotekelezwa chini ya Programu ya GPE LANES II kwenye elimu ambapo baadhi ya Halmashauri na Taasisi zimefanya vizuri ijapokuwa taasisi chache zilipata changamoto ya utekelezaji wa miradi.
Akitoa neno la shukrani Adam Shimatayo amemshukuru mgeni rasmi kwa kuwatia moyo kuendelea kufanya kazi pamoja na kutokuwa na hofu ya changamoto za elimu
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.