Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na halmashauri hiyo kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja wa miradi hiyo inayolenga kuboresha ustawi wa wananchi wa Dodoma.
Akiongelea lengo la ziara hiyo katika mradi wa ujenzi wa Soko la wazi la wafanyabiashara wadogo (Machinga), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema kuwa ziara hiyo ya kawaida ililenga kuwajengea uelewa wa pamoja wajumbe wa Menejimenti juu ya miradi inayotekelezwa na halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mafuru alisema kuwa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri inapotoka kwenda kutembelea miradi inawasaidia kutoa ushauri wa kitaalam katika miradi hiyo. Sababu nyingine aliitaja kuwa ni kuona utofauti uliopo baina ya mradi mmoja na mwingine.
Akiongelea ujenzi wa Soko la wazi la Machinga, Mkurugenzi huyo alisema kuwa ujenzi huo unatarajia kugharimu shilingi bilioni 7.5. “Wafanyabiashara wadogo wenyewe walichagua eneo hili kwa sababu ya urahisi wake kufikika” alisema Mkurugenzi Mafuru.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.