HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kusajili wananchama 258 katika siku yake ya pili ya zoezi maalum la uhamasishaji wananchi kujiunga na Bima ya Afya iliyoboreshwa CHF.
Akitoa taarifa ya zoezi hilo lililofanyika katika kata ya viwandani jana, mratibu wa CHF iliyoboreshwa Patrick Sebyiga alisema kuwa zoezi limekuwa na mafanikio.
Sebyiga alisema kuwa katika kata ya Viwandani, jumla ya kaya 43 zilisajiliwa. Kaya hizo zinawatu 258. Alisema kuwa hayo ni mafanikio makubwa katika uandikishaji wanachama kwa CHF iliyoboreshwa.
Mratibu huyo alisema kuwa katika kuboresha CHF katika vituo vya kutolea huduma na hospitali zote za serikali zimewekwa simu maalum kwa ajili ya kuhudumia wanachama wa CHF iliyoboreshwa kwa ufanisi.
Mhamasishaji wa usajili wanachama wa CHF iliyoboreshwa, Mysarah Maneno alisema kuwa ana wajibu wa kuhamasisha wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa kutokana na umuhimu wake. “CHF iliyoboreshwa ni bima rahisi na ya gharama nafuu, huduma ni nzuri pia. Kupitia CHF iliyoboreshwa sehemu yoyote kwenye vituo vya afya na hospitali za serikali nchini unapata huduma ya matibabu”.
Kwa upande wake mkuu wa kaya Frank Edson baada ya kujisajili na CHF iliyoboreshwa aliishukuru serikali kwa uamuzi huo. “CHF iliyoboreshwa inakupa uhakika wa matibabu katika hospitali. Bila CHF iliyoboreshwa ingekuwa usumbufu na gharama kubwa sana za matibabu” alisema Edson. Alitoa wito kwa wananchi ambao hawajajiunga na CHF iliyoboreshwa kujiunga mapema ili kunufaika na bima hiyo.
Wananchi wakipata maelekezo kuhusu CHF Iliyoboreshwa kutoka kwa maafisa wanaohusika na Bima ya Afya ya CHF iliyoboreshwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.