Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Patrick Sebyiga (pichani) amewapongeza wakazi wa Jiji hilo kwa kulifanya kuwa kinara katika zoezi la uandikishaji na utoaji wa kadi za huduma ya afya zilizoboreshwa.
Sebyiga aliyasema hayo katika zoezi la utoaji wa fedha za mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF), ambapo zoezi hilo liliambatana na uandikishaji wa wananchi wenye uhitaji na kadi za CHF iliyoboreshwa.
Alisema kuwa katika zoezi hilo walengwa wengi wamekuwa na mwamko wa kulipia kadi hizo kwa kuwaambatanisha na wategemezi wao hali inayowahakikishia upataji wa huduma za afya katika vituo vyote nchini.
"Kadi za CHF iliyoboreshwa zinapatikana kwa shilingi 30,000 (elfu thelathini) tu, ambapo anayeilipia anakuwa na wategemezi wake 5 jumla wanakamilisha idadi ya watu sita, na wanapopatiwa kadi hii wanakuwa na uhakika wa kupata huduma katika maeneo waliyopo" alisema Mratibu huyo.
Pia, ametoa takwimu ya watu waliojiandikisha kwa jiji zima la Dodoma ambapo amekiri zoezi la uandikishaji linaridhisha na kuwataka wananchi kuendelea kuhamasishana ili kila mmoja aweze kuwa mwanachama wa CHF.
"Hadi hivi sasa tumeandikisha kaya 6,325 na kaya moja wakishalipia wanakuwa jumla watu sita wanaopatiwa huduma, hivyo kwa idadi hii ya kaya, jumla tumeandikisha wanachama wapya 37,950.
Aidha, amewasisitiza wananchi ambao bado hajajiandikisha watambue mchango wa mifuko ya afya na kuwataka wajiandikishe ili waweze kuwa na uhakika wa kupatiwa huduma za kiafya pindi waendapo hospitali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.