Serikali ya Jimbo la Hunan imeanzisha mtaa maalum wa kuuza kahawa kutoka Barani Afrika katika soko kuu la Gaoquiao jijini Changsha. Hafla ya uzinduzi wa mtaa huo imefanyika leo na kuhudhuriwa na wawakilishi wa mataifa mawili ya Tanzania na Ethiopia yanayozalisha kahawa.
Hunan Galuiao Market ni soko la tatu kwa ukubwa nchini China linalouza bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya China. Uzinduzi wa mtaa wa kuuza kahawa kutoka Afrika ni sehemu ya hatua za Jimbo la Hunan kufungua soko lake kwa bidhaa kutoka barani Afrika.
Hafla hiyo ya ufunguzi wa mtaa kuuza kahawa ilifuatikwa na mkutano aw biashara uliohudhuriwa na washiriki 360 (onsite) na 2000 (online) ambapo Tanzania, Ghana na Ethiopia zilipata fursa ya kuwasilisha mada juu ya fursa za biashara ya mazao ya klimo na uwekezaji katika viwanda.
Balozi wa Tanzania, Mbelwa Kairuki ameyakaribisha makampuni ya Jimbo la Hunan kuwekeza nchini Tanzania kwa kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo yanayolimwa Tanzania ikiwa ni pamoja na korosho, pamba, katani, ufuta, muhogo, karanga na soya.
Chanzo: Azamtvtz (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.