SHULE ya sekondari Chinangali inatekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 kwa lengo la kutoa huduma bora.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa shule ya sekondari Chinangali, Mwalimu Victor Salisali alipokuwa akisoma taarifa ya uzinduzi wa mradi wa jengo la Utawala shule ya sekondari Chinangali kwa Kiongozi wa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 shuleni hapo.
Mwalimu Salisali alisema “pamoja na mambo mengine, shule inatekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru isemayo “‘TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu, itumie kwa usahihi na uwajibikaji”’ ambapo wanafunzi wote 1,182 waliopo shuleni hapo wamesajiliwa kwa kutumia mfumo wa TEHAMA uitwao PREM (Primary Record Enrollment Management). Mfumo huu pia hutumika kuhamisha wanafunzi. Aidha, shule inatumia mfumo wa TEHAMA wa FRARS (Facility Financial Accounting and Reporting System) kukiri mapokezi ya fedha inazopokea kutoka vyanzo mbalimbali, kufanya matumizi ya fedha hizo pamoja na kufanya usuluhisho wa kibenki. Hii inawezesha uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma” alisema Mwalimu Salisali.
Shule ya sekondari Chinangali ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa ni shule ya Kata ya Chamwino yenye jumla ya wanafunzi 1,182 wanaosoma kidato cha I-IV, na ikiwa na walimu 44.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.