WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amesema tafiti zitakazokuwa zikifanyika katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo jijini Dodoma zitakuwa na mchango mkubwa katika medani za kitaifa na kimataifa na ufanisi wa utendaji kazi katika mamlaka za serikali za mitaa hapa nchini.
Waziri Jafo alisema hayo jana Agosti 13, 2020 katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo jijini Dodoma kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ujenzi wa kumbi za kufundishia pamoja na uzinduzi wa nyumba za watumishi .
Pia alisema kuwa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kimeendelea kukua kutokana na serikali ya awamu ya tano kuongeza juhudi katika kukipanua chuo hicho hususan kiwango cha elimu kutoka Stashahada hadi Shahada pamoja na uimarishaji wa miundombinu.
Aidha, Waziri Jafo amewataka wanafunzi wanaosoma chuo cha serikali za mitaa Hombolo kusoma kwa bidii hasa wale ambao ni waanzilishi wa elimu ngazi ya shahada (Degree) na wakawe mfano kwa wengine.
Katika hatua nyingine, Waziri Jafo ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kufuata maagizo yake ya kujenga kwa kutumia mfumo wa manunuzi ya umma yaliyokubalika kisheria ya haraka na gharama nafuu katika kazi za ujenzi (Force Account) kwani hali hiyo imeokoa zaidi ya Tsh. Milioni mia saba.
Naye Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dkt. Martine Madale amesema kila darasa lina uwezo wa kukaa wanafunzi 250 na mpango ilitakiwa kutumia zaidi ya Tsh. milioni 625 lakini kwa kutumia mfumo wa 'Force Account' wanatarajia kutumia zaidi ya Tsh. Miliomi 274 pekee.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.