Mkutano wa 19 wa Bunge la kumi na moja ambao ni mahsusi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Serikali utaanza Jumanne tarehe 31 Machi 2020 na kuendelea hadi tarehe 30 Juni 2020.
Hayo yamesemwa katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Ofisi ya Bunge leo 30 Machi 2020 na kutoa ufafanuzi wa jinsi bunge bunge hilo litakavyoendeshwa.
Kufuatia janga la ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona utaratibu wa uendeshajji wa shughuli za Bunge katika Mkutano huu utakuwa tofauti na ilivyozoeleka. Kwa mujibu wa Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Mb), mabadiliko yafuatayo yatafanyika ikiwa ni hatua za kujikinga na ugonjwa wa Corona wakati wa vikao vya Bunge.
Mosi, uda wa vikao vya Bunge utapunguzwa kutoka saa tisa kwa siku hadi saa nne ambapo; vikao vitakuw vikifanyika kuanzia saa 8:00 Mchana ahdi saa 12:00 Jioni. Hata hivyo mabadiliko ya muda hayatahusu kikao cha kwanza ambacho kilishapangwa toka awali kuanza saa tatu.
Pili, idadi ya Wabunge watakaoingia Bungeni imepunguzwa ambapo katika Mkutano huu, Wabunge watakaokuwa wanaingia ndani ya Ukumbi wa Bunge hawatazisdi mia na hamsini (150) kwa wakati mmoja. Wabunge watakaoingia Bungeni ni wafuatao:
• Mhe. Spika
• Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni
• Kiongozi wa Kamba Rasmi ya Upinzani Bungeni
• Wanadhimu wa kila Chama
• Mawasili na Manaibu Mawaziri
• Mwanasheria Mkuu wa Serikali
• Mawaziri Vivuli na Manaibu wao
• Wajumbe wa Kamati ya Uongozi
• Wajumbe wa Tume ya Bunge
• Kamati ya Bajeti, na
• Makamu Wenyeviti wa Kamati
Waheshimiwa Wabunge ambao hawataingia ndani ya Ukumbi wa Bunge watafuatilia Shughuli za Bunge kupitia runinga katika Kumbi na maeneo mengine yaliyopangwa.
Tatu, kufuatia utaratibu huu mpya Waheshimwa Wune watauliza maswali na kujibiwa kwa njia ya maandishi kupitia tablet zao. Katika utaratibu huu Wabunge wote watatumiwa maswali na majibu, na Mbunge mwenye swali la misingi ataruhusiwa kuuliza maswali ya nyongeza kwa njia ya maandishi kupita tablet. Vilevile hakutakuwa na kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Nne, kuhusu utaratibu wa upigaji kura wakati wa kupitisha Bajeti za Wizara Waheshimiwa Wabunge watapiga kura kwa njia ya mtandao kupitia Tablet zao isipokuwa wakati wa upitishaji wa Bajeti Kuu ya Serikali ambapo Wabunge wote watapata fursa ya kupiga kura ya wazi kwa kuita jina la Mbunge mmoja mmoja. Pamoja na hayo waheshmiwa Wabunge watakuwa pia na uwezo wakuchangia katika mijadla ya Bajeti, Miswada na Maazimio kwa anji aya maandishi kupitia Tablet zao.
Kwa mujibu wa Mhe. Spika mabadiliko haya ni ya muda kufuatia ugonjwa wa Corona. Hivyo mabadiliko mengine yanaweza kufanyika au haya yakaondolewa kwa kuzingatia hali itakavyokuwa.
Kusoma taarifa kamili bofya hapa: Bunge - Taarifa kwa Umma.pdf
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.