Mamia ya wasafiri waliokuwa wakisafiri kati ya mikoa ya Morogoro na Dodoma na maeneo jirani leo Jumatatu Machi 2, 2020 wamejikuta wakikwama kuendelea na safari zao kutokana na kuchukuliwa na maji daraja la Kiyegeya lililopo eneo la Magubike.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 9 alasiri na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria waliokuwa katika mabasi na magari binafsi kukwama eneo hilo.
Kufuatia kadhia hiyo, baadhi ya watu walilazimika kugeuza na kutumia njia mbadala kuendelea na safari.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare akizungumzia tukio hilo na suluhisho la haraka kwa muda huu amesema mabasi ya abiria na magari madogo yanayotumia barabara ya Morogoro kwenda Dodoma ameshauri kutumia njia mbadala ya kupitia Iringa.
Amesema kuwa hadi kufikia saa 12 jioni wataalam mbalimbali wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kuanza matengenezo mara moja. Aidha, yeye pamoja na kamati ya ulinzi na usalama watakwenda eneo la tukio na kusema kwamba hakuna vifo wala majeruhi walioripotiwa kwenye tukio hilo.
“Sasa hivi askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wanaelekea katika eneo hilo kwa ajili ya matengenezo,” amesema RC Sanare.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.