Na. Leah Mabalwe, DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj. Jabir Shekimweri atoa agizo la ukamilishaji wa shule ya msingi Mayeto ifikapo tarehe 8 Januari, 2023 mara baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa mradi huo uliopo Kata ya Hombolo Makulu.
Alitoa agizo hilo alipotembelea shule hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya shule mpya na shikizi inayoendelea ndani ya Wilaya ya Dodoma.
’’Nimetembelea miradi mingi ya shule lakini nimekuja katika kata hii ya Hombolo Makulu naona kabisa kuna mapungufu katika umaliziaji wa mradi huu wa shule ya msingi Mayeto, kwahiyo nawapa muda kuanzia leo hadi tarehe 8 Januari,2024 mradi uwe umekamilika ikiwemo kurekebisha maeneo yote ambayo nimeyabainisha. Nimewapa muda huu kwasababu nataka mradi ukamilike kwa wakati ifikapo Jumatatu tarehe 8 shule zinapofunguliwa wanafunzi watumie majengo haya’’ alisema Alhaj Shekimweri.
Kwaupande wake Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, Issa kambi, aliahidi kuongeza usimamizi na kuhakikisha marekebisho yanafanyika na kukamilika kwa wakati pia kuleta vifaa kwaajili ya umaliziaji na urekebishaji wa shule hiyo.
“Tumeshabaini makosa mbalimbali na tumeshaanza kuyafanyia kazi katika shule hii pia, Mkurugenzi wa Jiji ameshatuma wataalam kuja kutathmini marekebisho yanayotakiwa katika shule hii ya Mayeto na tayari tumetenga kiasi cha fedha kwaajili ya marekebisho hayo ya shule. Hadi sasa vitu vya kufanyia marekebisho ya shule tayari vimeshanunuliwa hivyo, ifikapo ijumaa vitu vyote vitakuwa tayari vimeshafanyiwa marekebisho’’ alisema Kambi
……”Tumegundua pia kuna upungufu wa nguvu ya usimamizi hapa kwahiyo tumeamua kuongeza nguvu kazi kutoka ofisi ya mkurugenzi kwaajili ya usimamizi na kuhakikisha unakamilika kabla ya shule kufunguliwa’’ aliongezea
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.