Dc Shekimweri afanya ziara katika soko la Machinga
Imewekwa tarehe: December 3rd, 2024
Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri amefanya ziara katika soko la Machinga kwa Lengo la kukagua miundombinu ya maji,umeme na mawasiliano Katika soko hilo.
Shekimweri alifanya kikao na viongozi wa soko pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuagiza utekelezaji wa maboresho ya miundombinu mibovu sokoni hapo.
Aidha, Shekimweri amesisitiza uwajibikaji Kwa wazabuni wote waliopo Katika soko la Machinga ili kuondokana na kero zinazotolewa na wafanya biashara wa sokoni hapo.