Na Getruda Shomi, DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri (wa kwanza kushoto pichani juu) ametoa mapendekezo ya kuongeza vivutio, kuweka teknolojia rafiki ya ulinzi ili kulinda usalama wa watu na mali zao na kuwavutia zaidi wateja kutembelea bustani hiyo ya kupumzikia na kuongeza mapato.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa mapendekezo hayo katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika Wilaya ya Dodoma kuona namna miradi hiyo inavyoendeshwa na maendeleo yake alipotembelea Bustani ya Mapumziko ya Chinangali.
Mhe. Shekimweri alipendekeza kuongeza vivutio vya wanyama na kuwepo kwa teknolojia rafiki kwa ajili ya kulinda usalama wa watu na mali zao wawapo katika eneo hilo. Pendekezo lingine ni wawepo wataalam wa kuogelea ili kufundisha watu namna ya kuogelea lakini pia kufanya uokozi pindi inapotaka kutokea ama inapotekea ajali ya mtu kuzama.
Aidha, Shekimweri alimtaka Meneja wa Bustani ya Mapumziko Chinangali kuwekeza zaidi kwenye huduma kwa wateja. “Lazima tuhakikishe tunaweka kitu cha kiupekee ambacho mtu hawezi kukipata kwenye sehemu nyingi yeyote” alisisitiza Shekimweri.
Bustani hiyo ya mapumziko, ipo mkabala na Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Dodoma ikitengenishwa na barabara kuu iendayo Arusha.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.