Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini, Jabir Shekimweri (mwenye kofia pichani juu) amepiga marufuku kitendo cha wapiga debe na bodaboda Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma kulazimisha abiria wanaokwenda mjini kuwashushia kituoni hapo hata kama hawana uhitaji wa kushukia kwenye kituo hicho.
Marufuku hiyo ameitoa alipofanya ziara kituoni hapo baada ya kupokea malalamiko ya baadhi ya abiria kuwa wamekuwa wakilazimishwa na wapiga debe kushukia Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma ili wapande bodaboda licha ya kuwepo mabasi ya mikoani yanayopitiliza mpaka mjini kati Dodoma.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea eneo lenye ukubwa wa ekari nane lililotengwa kwa ajili ya wajasiliamali lililopo katikati ya Kituo ya Kikuu cha Mabasi na Soko Kuu la Job Ndugai na kutoa ushauri namna nzuri zaidi ya upanuzi wa maeneo ya wajasiriamali huku mbunge wa jimbo la Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde akizungumzia manufaa yatakayopatikana kutokana na eneo hilo.
Awali akitolea maelezo juu ya eneo hilo la wajasiriamali, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Jiji la Dodoma Hidaya Mizega amesema katika eneo hilo kutakuwa na kiwanda cha kusindika maziwa na ngozi huku Mstahiki Meya Prof. Davis Mwamfupe akisema hatua hiyo ni namna bora ya baraza la madiwani kutumia asilimia 10 ya mkopo ambapo Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Dodoma Inspekta Deogratius Inano akisema ni muhimu jeshi hilo kushikikishwa pia.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Jiji la Dodoma Hidaya Mizega akitoamaelezo kuhusueneolitakalotumiwanawajasiriamali.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri (wa tatu kutoka kulia) akimsikiliza Mhandisi wa Jiji la Dodoma, QS Ludigija Ndatwa akielezea hatua za ukamilishaji wa eneo la wajasiriamali na taratibu wa uendeshaji wa huduma mbalimbali katika Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma, kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.