• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

DC Shekimweri apongeza Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma

Imewekwa tarehe: February 28th, 2025

Na. Aisha Ibrahim, VIWANDANI

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kurejesha tena Kliniki ya Ardhi inayolenga kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi zinazohusiana na masuala ya Ardhi.

Pongezi hizo alizitoa wakati wa ufunguzi wa zoezi la Kliniki ya Ardhi lililoanza leo na kuendelea mpaka tarehe 28 Februari, 2025, eneo la Halmashauri ya Manispaa ya zamani, jijini Dodoma.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa kliniki hiyo, Alhaj Shekimweri alisema kuwa ni vema kufanya tathmini ya kero mbalimbali za Ardhi zilizopita na kuzitafutia ufumbuzi kabla ya kusikiliza kero mpya kwasababu itakuwa ni sawa na kufanya kazi bure kuzungumzia kero moja kila wakati. “Ni vema kufanya tathmini ya mazoezi yaliyopita kwasababu pengine kuna mtu zoezi lililopita alikuwepo na hili yupo kwa changamoto ile ile, huenda hajaridhika na huduma au majibu aliyoyapata kliniki iliyopita ndiyo maana yupo tena” alisema Alhaj Shekimweri.

"Wataendelea kuja kama wanaowashughulikia ni miongoni kwa visababishi vya matatizo yao, yaani mtu anayo kero ya miliki pandikizi alafu anayeishughulikia ndiye aliyesababisha kupatikana kwa kero hiyo kwahiyo tegemea kumuona kila kliniki kwa changamoto ile ile lakini pia mnakubaliana kwenda 'site' na baadae inasitishwa kwahiyo jambo lake ni kama litaanza tena upya, hivyo hapa atakuja mara kwa mara” aliongeza.

Sambamba na hilo alisema, ni lazima kuwepo na dawati maalum la kupokea na kusimamia maoni ya wananchi kwa lengo la kukusanya kero na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wananchi kwasababu jambo hilo litaepusha kupunguza msongamano wa kero zinazojirudia kila wakati. “Kuwepo na dawati la kusikiliza na kupokea maoni yetu na ushauri kwasababu tangu nimefika hapa nimepokea maoni mengi na ni mazuri” alisema Alhaj Shekimweri.

Aidha, alikemea kitendo cha wasimamizi wa Ardhi kushindwa kutimiza majukumu yao kwa wakati kwa kusingizia changamoto ya mtandao na aliwataka kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa haraka iwezekanavyo. “Kuna watu hapa wanataka kusoma, kuangalia hiyo migogoro na hatimiliki mitandaoni, nunueni mtandao wa kisasa wa bila nyaya 'Wi-Fi' na muweke bango kubwa sehemu hii lililoandikwa msimbo ili kila mwenye shida ya mtandao aweze kutatua shida hiyoo na kuepuka visingizio” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, aliomba wazee, wajawazito na watu wenye ulemavu kupewa kipaumbele   na kutengewa eneo maalum katika kliniki hiyo. “Wazee, wajawazito na watu wenye ulemavu wapewe kipaumbele katika huduma hii pia watengewe meza maalum, kwahiyo wazee hawa wasiendelee kuomba hisani kwaajili ya kuhudumiwa kwasababu hatupo hapa kufanya biashara” alisema.

Lakini, aliwasisitiza wananchi kuwa na nyaraka zenye uthibitisho wa eneo analolishughulikia kwasababu maneno bila uthibitisho ni mojawapo ya sababu ya kujirudia kwa kero mbalimbali za Ardhi katika kila kliniki. “Hatuwezi kushughulikia mgogoro ambao mtu anaongea tu bila nyaraka au uthibitisho halisi, mara oooh! Niliuziwa na mauziano hayapo, mara nilitapeliwa kiwanja changu na hakuna nyaraka yoyote” alisisitiza Shekimweri.

Alimaliza kwa kushauri kuwa, wananchi wapatiwe elimu ya kutosha kuhusu haki zao na hatimiliki kwa kufuata misingi ya kisheria ili kuondoa migogoro ya Ardhi na kama hatoridhika na maamuzi ya mahakama anayo haki ya kukata rufaa ilimradi haki msingi ipatikane.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.