MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri ameyataka makampuni yaliyopata kandarasi ya usafi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kufanya kazi hiyo kwa kiwango na kuhakikisha jiji linakuwa safi ili kuwaepusha wananchi dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Agizo hilo alilitoa wakati akiongea na wamiliki wa makapuni ya usafi waliopata kandarasi ya kufanya usafi katika Jiji la Dodoma na wananchi waliojitoleza katika zoezi la usafi lililofanyika katika kata ya Kikuyu Kaskazini leo.
Shekimweri alisema “nawapongeza kwa kupewa kandarasi hii, lakini nawapa pole kwa sababu kwa kweli tutakuwa wakali sana kwenye changamoto tunayokuta kwenye maeneo mengi ya kuzagaa kwa taka. Wananchi hawa rahimu wana muitikio kama huu watafanya usafi na kupeleka kwenye ‘collection point’ na nyie mchukue hamuendi kuchukua. Katika hili tutagombana sana. Mkurugenzi nimefurahi umewapatia mkataba wa mwaka mmoja makusudi ili tuwapime. Nataka Mkurugenzi usimamie mkataba ule vizuri”.
Akijibu swali kuhusu maeneo ya viwanja ambavyo havijaendelezwa na kugeuzwa kuwa maeneo ya kutupwa takataka, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema kuwa maeneo hayo yatafutwa. “kuhusu mapagale na vichochoro, nitatuma timu ya wataalam Jumatatu itembelee mitaa yote kuanza na Kikuyu. Tuangalie viwanja gani vipo wazi, viwanja gani vinamapale ambayo hayajakamilika na vichochoro. Kwa wenye viwanja ambavyo hawajaendeleza walipewa miezi 36 kuwa wameviendeleza. Tutaorodhesha viwanja hivyo na kupeleka kwenye kamati ya ugawaji wa Ardhi na kupeleka kwa Kamishna vifutwe kwa ajili ya watu wenye nia ya kuendeleza” alisema Mkurugenzi Mafuru.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu, Dickson Kimaro alisema kuwa suala la usafi ni ustaarabu. Aidha, aliyataja makampuni yaliyopata kandarasi ya usafi kuwa ni Al Jabry Investment iliyopewa kata ya Uhuru na Kiwanja cha Ndege. JKT Suma Cleaning and Fumigation imepewa Kata ya Viwandani, Makole, Tambukareli, Madukani. Kampuni ya tatu aliitaja kuwa ni Wejisa Company Ltd iliyopewa Kata ya Majengo na Kilimani.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.