MKUU wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dodoma na maeneo ya jirani kujitokeza katika mkesha wa Kitaifa wa kuliombea Taifa amani utakaofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma usiku wa Disemba 31, 2021 huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye atawakilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Paramagamba Kabudi.
Kamati ya maandalizi ya mkesha huo ulioandaliwa na makanisa kadhaa nchini imekutana na waandishi wa Habari jijini Dodoma leo Disemba 29, 2021 katika hoteli ya 56 ambapo mwakilishi wa Mkuu huyo wa Wilaya Lucas Mbise alisema tukio hilo lililoandaliwa na viongozi wa dini ya Kikristo ni muhimu kwa Taifa kwani amani na utulivu ndo msingi wa maendeleo na kwamba Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itatoa ushirikiano wote katika kufanikisha tukio hilo linalofanyika kwa mara ya kwanza katika Makao Makuu ya Nchi.
Mwenyekiti wa kamati ya maadalizi ya tamasha hilo Askofu Godfrey Mallasy alisema maandalizi yamekamilika ikiwemo kupata vibali husika na kwamba tamasha hilo lilianza mwaka 1997 jijini Dar es salaam ambapo mwaka 2006 lilianza kufanyika katika uwanja wa Uhuru na baadaye kusambaa mikoani mwaka 2018 na hadi sasa linafanyika katika mikoa kadhaa ya Tanzania Bara pamoja na Zanzibar ambapo rasmi atakuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Askofu Mallasy alitoa wito kwa Wakristo na Watanzania kwa ujumla kuitikio wito wa kushiriki katika tamasha hilo la mkesha wa kuiombea nchi Kitaifa kwani kila mtu anahitaji amani katika maisha yake.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.