WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanadhibiti magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu na homa ya nyani.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa mkutano wa tathimini ya mkataba wa lishe na kutambulisha mpango wa taifa wa uwekezaji katika afya ya mama na matoto nchini.
Alisema kwa sasa ugonjwa wa kipindupindu umeendelea kuenea na umechukua muda mrefu kudhibitiwa katika mikoa ya Simiyu, Songwe, Mbeya, Mwanza, Tabora, Dodoma, Lindi, Mara, Kigoma, Arusha na Tanga.
“Niwaombe sana wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya na watendaji ngazi zote mukawe mstari wa mbele kuudhibidi na kuutokomeza kabisa ugonjwa huu.”
“Mkoa wa Simiyu unaoongoza kwa ugonjwa kuwepo na wagonjwa 25 hadi 40 kwa siku wa kipindupindu, Meatu wako wapi (wanaongoza) nawapa wiki tatu mwende mkamalize kipindipindu na mkasisitize matumizi ya vyoo.”
Kwa mikoa ambayo haijaripoti uwepo wa wagonjwa wa kipindupindu kwa sasa mukaimarishe afua za kujikinga na gonjwa huu wa aibu. Mikoa ambayo haijawahi kuripoti wagonjwa wa kipindupindu ni Mkoa wa Njombe na Iringa.”
Kwa upande wa ugonjwa wa homa ya nyani(M-POX), Mhe. Mchengerwa ameitaka mikoa yote hasa ya mipakani na inayopokea wasafiri wageni kutoka nchi ziliothibitisha kuwa na ugonjwa huo kuchukua hatua madhubuti za afua za afya kinga ikiwemo kuzingatia kanuni zote za kujikinga na kudhibiti Ugonjwa huu.
“Kwa sasa nchi yetu iko salama hadi sasa dhidi ya Ugonjwa huu ila nawaomba viongozi na watendaji ngazi za mikoa, wilaya na halmashauri mukasimamie kikamilifu afua za afya kinga dhidi ya Ugonjwa wa M-Pox.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.