Na. Dennis Gondwe, DODOMA
DIWANI wa Kata ya Kikombo, Emmanuel Manyono amepongeza mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuzingatia kukamilisha ujenzi wa miradi viporo ili kuunga mkono juhudi za wananchi.
Pongezi hizo alizitoa alipokuwa akichangia juu ya mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
“Nianze kuipongeza rasimu ya mapendekezo ya Mpango na Bajeti hii ya mwaka 2024/2025. Bajeti hii tumeichakata kuanzia katika vikao vyetu vya kamati. Bajeti hii ukiifuatilia, kwanza imezingatia sana miradi ya maendeleo ya wananchi hasa inayoibuliwa na wananchi na kuanza kuitekeleza. Pili imezingatia kumalizia vile viporo vya miradi. Kuna miradi mingi ilikuwa imekwama katika kata zetu, lakini miradi hiyo kwenye bajeti hii imewekwa ili iweze kukamilishwa mwaka huo wa fedha na iendelee kutoa huduma kwa wananchi” alisema Manyono.
Akiongelea kuongezeka maeneo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, alisema ongezeko hilo ni muhimu kwa wananchi. “Kwenye bajeti hii kuna maeneo yameongezwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Maeneo haya yaliyoongezwa yanakwenda kuinua vipato vya wananchi wetu ili waishi maisha mazuri” alisema Manyono.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.