Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi jana ametangaza mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake kuwa, amepokea barua ya kujiuzulu Diwani wa Kata ya Kizota Jamal Yared Ngalya kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Pamoja na kujiuzulu huko, Jamal amefanya maamuzi ya kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichokuwa mwanachama wake kabla ya kujiunga na CHADEMA kisha kugombea nafasi ya udiwani na kushinda katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Katika barua yake, Jamal ametoa sababu za kurejea CCM kuwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, jinsi anavyokiendesha Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake.
Aidha, Mkurugenzi Kunambi alitoa ufafanuzi kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya Madiwani 60 ambapo kati yao, 51 ni wa chama tawala CCM na madiwani 9 ni wa CHADEMA.
Kufuatia kujiuzulu Mh Jamal, Kata ya Kizota inakuwa wazi na taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa mujibu wa maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.