NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amefungua rasmi maonesho ya Wiki ya Nishati katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma ambapo amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha Sekta ya Nishati kutokana na nyenzo na maelekezo anayoyatoa ambayo yamempambanua kama kiongozi anayetatua matatizo ya wananchi kwa kutenda zaidi na sio maneno.
Dkt. Biteko amesema maelekezo ya Rais, Dkt. Samia pamoja na nyenzo anazozitoa kwa Wizara ya Nishati zimepelekea nchi sasa kuwa na umeme wa kutosha na kwamba hakuna mgawo tena huku kukiwa na mitambo ambayo ipo standby kuwashwa pale inapotokea hitilafu kwenye mitambo mingine ya uzalishaji umeme.
Aidha, kwa mikoa ambayo ipo nje ya gridi ya Taifa ikiwemo Katavi, Rukwa, Kigoma, Lindi na Mtwara, amesema kuwa yote itaunganishwa kwenye gridi ya Taifa kwani Rais, Dkt. Samia ameshatoa fedha za kutekeleza miradi ya umeme itakayoiunganisha mikoa hiyo na gridi ambayo tayari inaendelea.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ameipongeza TANESCO kwa kuendelea kuimarisha utendaji kazi wao ikiwemo utatuzi wa changamoto za umeme akitolea mfano athari iliyotokea katika gridi ya umeme usiku wa siku ya Pasaka kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa kudhibiti kiwango cha maji kwenye mitambo ya Kidatu ambapo tatizo hilo lilipaswa kushughulikiwa kwa siku tatu lakini TANESCO ilifanya jitihada na kutatua changamoto hiyo kwa muda wa masaa kadhaa.
Pamoja na pongezi hizo Dkt. Biteko ametoa angalizo kwa kampuni tanzu za TANESCO kuhusu utendaji kazi wao ikiwemo Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) ambapo kampuni hiyo ilitoa ahadi ya kuanza uchorongaji wa visima vya Jotoardhi katika eneo la Ngozi Mbeya tarehe 1 Aprili 2024 lakini bado hawajaanza kazi hiyo hivyo amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati kuisimamia ipasavyo kampuni hiyo ili nchi iweze kupata umeme wa Jeothemo.
Pamoja na uendelezaji wa Sekta ya Umeme, Dkt. Biteko amesema kuwa Wizara inaendelea na utekelezaji wa mipango mingine ikiwemo wa nishati safi ya kupikia ambapo Baraza la Mawaziri limeshapitisha Mpango Mkakati wa Nishati safi ya kupikia na sasa kinachofanyika ni utekelezaji
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.